Tafuta katika Blogu Hii

Ijumaa, 21 Septemba 2018

Mosri Tv...Updates : WALIOFARIKI KWENYE AJALI YA KIVUKO KUZAMA ZIWA VICTORIA WAFIKIA 44..RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI

Seebait.com 2018SeeBait

Mpaka usiku huu jumla ya watu 44 wanaripotiwa kufariki dunia na wengine 37 kuokolewa baada ya Kivuko cha MV Nyerere mkoani Mwanza kinachofanya safari kati Bugorora katika Kisiwa cha Ukerewe na Kisiwa cha Ukara katika Ziwa Victoria kuzama leo Alhamis Septemba 20,2018 mchana katika ziwa Victoria.

Kwa Mujibu wa Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella Zoezi la uokoaji wa abiria waliokuwemo katika kivuko cha MV Nyerere limesitishwa kutokana na giza, na litaendelea kesho alfajiri ambapo hadi sasa waliyookolewa wakiwa hai ni 37, waliokufa 44. 

Rais John Magufuli ametuma salamu za rambirambi na pole kutokana na ajali ya kivuko cha Mv Nyerere.

Usiku huu wa saa 20.40, Rais Magufuli ametoa salamu hizo kupitia kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais- Ikulu, Gerson Msigwa aliyepiga simu Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wakati wa taarifa ya habari.

“Rais anatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki waliofikwa na ajali,” amesema Msigwa

Msigwa amesema, “Rais anaomba Watanzania kuwa watulivu wakati juhudi za uokoaji zinaendelea na baadaye Serikali itaweza kutoa taarifa cha nini kitakachoendelea.”

Msigwa amesema taarifa ambazo Rais Magufuli amezipata kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela zinasema, Kwamba zaidi ya watu 40 wameokolewa.”

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shana amesema kivuko hicho kimezama leo mchana baada ya kupinduka. “Kiliondoka saa 6 mchana na ilipofika saa nane kamili mchana kilipinduka,” amesema.

Kivuko hicho kilikuwa kinatoka Bugorora kwenda Ukara katika Ziwa Victoria kimezama kikidaiwa kuwa na watu zaidi ya 100 huku ikidaiwa kuwa ni kawaida kwa kivuko hicho kubeba watu wengi siku za Alhamis kutokana na kuwepo kwa gulio.

Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), Hassan Karonda amekiri kuzama kwa kivuko hicho Kivuko hicho cha Mv Nyerere kina uwezo wa kubeba abiria 100, tani 25 za mizigo na magari madogo matatu

Jumamosi, 31 Machi 2018

MAGAZETI

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI YA MARCH 31,2018

Seebait.com 2018VICHWA VYA HABARI KUU LEO JUMAMOSI TAR.31/.04/2018SeeBait

Ni asubuhi nyingine tena na habari kubwa kwenye Magazeti ya Tanzania March 31 2018 kuanzia ya, Udaku, Michezo na Hardnews kujionea yote makubwa yaliyoandikwa
USISAHAU KUDOWNLOAD APP YETU BURE HAPO JUU


Published from: MOSRI Tv

Jumatatu, 26 Februari 2018

MATOKEO KIDATO CHA NNE 2017/18

http://www.tamisemi.go.tz/noticeboard/tangazo-1096-20180130-Matokeo-kidato-cha-nne-2017/CSEE%202017/results/p0116.htm

MPWAPWA SEC. SCHOOL


Serikali yatoa kiasi cha bil 1.2 kwa ajili ya ukarabati wa shule kongwe mkoani Dodoma (MPWAPWA SEC)

Mapema septemba mwaka 2017 aliekuwa naibu waziri TAMISEMI
Ndugu Seleman Jaffo alifika shuleni hapo kukagua namna ukarabati huo unavyoendelea......Ambapo alimpongeza mkuu wa shule na mhandisi msimamaizi
wa mradi huo.......


Mpwapwa secondary ni moja kati ya shule kongwe zinazofanyiwa ukarabati wa kina.......

Licha ya shule hio pia Shule kama MUSOMA TECH.....TABORA BOYS.....pia ziko katika mpango huo wa ukarabati

Source; (Moses John)M.C.A Tv